Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele.Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu.Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.