Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”