Zaburi 67

Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

뉴스레터 구독

새로운 프로필과 행사, 플랫폼 소식을 받아 보세요.