Zaburi 128

Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake. Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana. Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

뉴스레터 구독

새로운 프로필과 행사, 플랫폼 소식을 받아 보세요.