Zaburi 121

Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

뉴스레터 구독

새로운 프로필과 행사, 플랫폼 소식을 받아 보세요.