Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:wazao wa Paroshi 2,172wazao wa Shefatia 372wazao wa Ara 775wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812wazao wa Elamu 1,254wazao wa Zatu 945wazao wa Zakai 760wazao wa Bani 642wazao wa Bebai 623wazao wa Azgadi 1,222wazao wa Adonikamu 666wazao wa Bigwai 2,056wazao wa Adini 454wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98wazao wa Besai 323wazao wa Yora 112wazao wa Hashumu 223wazao wa Gibari 95watu wa Bethlehemu 123watu wa Netofa 56watu wa Anathothi 128watu wa Azmawethi 42wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743wazao wa Rama na Geba 621watu wa Mikmashi 122watu wa Betheli na Ai 223wazao wa Nebo 52wazao wa Magbishi 156wazao wa Elamu ile ingine 1,254wazao wa Harimu 320wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 725wazao wa Yeriko 345wazao wa Senaa 3,630Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973wazao wa Imeri 1,052wazao wa Pashuri 1,247wazao wa Harimu 1,017Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74Waimbaji: wazao wa Asafu 128Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao wa // Shalumu, Ateri, Talmoni, // Akubu, Hatita na Shobai 139Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,wazao wa Uza, Pasea, Besai,wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,wazao wa Nesia na Hatifa.Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.Watumishi wa Hekalu wote na // wazao wa watumishi // wa Solomoni 392Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:wazao wa // Delaya, Tobia na Nekoda 652Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,ngamia 435 na punda 6,720.Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.