Esta 10

Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali. Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi? Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, akipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake, na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

뉴스레터 구독

새로운 프로필과 행사, 플랫폼 소식을 받아 보세요.