Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa: Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.Wana wa Yeduthuni walikuwa sita: Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.Wana wa Hemani walikuwa: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme.Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288.Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, // wanawe na jamaa zake, 12 Ya pili ikamwangukia Gedalia, // yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12Ya tatu ikamwangukia Zakuri, // wanawe na jamaa zake, 12ya nne ikamwangukia Isri, // wanawe na jamaa zake, 12ya tano ikamwangukia Nethania, // wanawe na jamaa zake, 12ya sita ikamwangukia Bukia, // wanawe na jamaa zake, 12ya saba ikamwangukia Yesarela, // wanawe na jamaa zake, 12ya nane ikamwangukia Yeshaya, // wanawe na jamaa zake, 12ya tisa ikamwangukia Matania, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi ikamwangukia Shimei, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na moja ikamwangukia Azareli, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, // wanawe na jamaa zake, 12Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, // wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, // wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini ikamwangukia Eliatha, // wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, // wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, // wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, // wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, // wanawe na jamaa zake, 12.