Zaburi 127

Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure. Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake. Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake. Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

Unseren Newsletter abonnieren

Bleiben Sie über neue Profile, Veranstaltungen und Plattform-Updates informiert.