Zaburi 87

Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

الاشتراك في نشرتنا الإخبارية

ابقَ على اطلاع بالملفات الجديدة والفعاليات وتحديثات المنصة.