Zaburi 114

Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni, Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake. Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma, milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo? Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo, aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

Neno: Biblia Takatifu

copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc — CC-BY-SA-4.0 — CC-BY-SA-4.0

Misoratra ao amin'ny gazety anay

Mahafantara hatrany ny mombamomba vaovao, ny hetsika ary ny fanavaozana ny sehatra.